Proverbs 1:25-30


25 akwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,

26 bmimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:

27 cwakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.


28 d“Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.

29 eKwa kuwa walichukia maarifa,
wala hawakuchagua kumcha Bwana,

30 fkwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
na kukataa maonyo yangu,
Copyright information for SwhKC